Habari

Imewekwa: Jan, 10 2024

MAFUNZO YA WARATIBU WA GEF

News Images

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Seif Shekalaghe amefunga Mafunzo ya Siku Mbili ya Waratibu wa Utekelezaji wa Programu ya Ahadi za Nchi Katika Kizazi Chenye Usawa, Januari 9, 2024, Jijiji Dar-es Salaam kwa kutoa rai kwa waratibu hao ambao ni Maafisa Maendeleo ya Jamii ‘Kuratibu na Kusimamia Programu hiyo kwa kuzingatia mila na maadili ya Kitanzania bila kusahau kuonyesha uwepo wao kila wanapopata nafasi wakati wanatekeleza majukumu yao ili kuipa thamani kazi yao.