Matangazo
Imewekwa:
Apr 01, 2022
TAARIFA MUHIMU KUHUSU MATOKEO YA MTIHANI VYUO VYA MAENDELEO YA JAMII
TAARIFA MUHIMU
Wizara inawatangazia wanafunzi wote wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii vya Uyole, Rungemba, Ruaha, Buhare, Mlale na Monduli na Vyuo vya Maendeleo ya Jamii Ufundi vya Misungwi na Mabughai kuwa matokeo ya Muhula wa kwanza kwa mwaka wa masomo 2021/2022 yametoka na yanapatikana katika tovuti www. jamii.go.tz na tovuti za Vyuo husika.
Wanafunzi ambao hawajafanya mitihani ya muhula wa kwanza watafanya mitihani maalum (special examination) baada ya muhula wa pili kukamilika.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini