Matangazo

Imewekwa: Jan 10, 2024

​TARATIBU ZA KUSAJILI MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI (NGOs) TANZANIA BARA

TARATIBU ZA KUSAJILI MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI (NGOs) TANZANIA BARA

A. MASHIRIKA YA NDANI YA NCHI (LOCAL NGO):-

(i) Lazima kuwe na watu wasiopungua watano (5) wote watanzania;

(ii) Kuwasilisha Katiba itakayosajiliwa;

(iii) Kuwasilisha Muhtasari wa kikao uliosainiwa na wanachama waanzislishi;

(iv) Kuwasilisha barua ya utambulisho (Recommendation Letter) kutoka kwa Msajili Msaidizi wa Halmashauri au Mkoa Ofisi ilipo.

B. MASHIRIKA YA KIMATAIFA (INTERNATIONAL NGO)

(i) Kuwa na watu wasiopungua watano (5) ambapo kati yao angalau wawili lazima wawe Watanzania;

(iii) Kuwasilisha nakala ya katiba ya usajili kutoka nchi iliposajiliwa;

(iv) Kuwasilisha nakala ya cheti cha usajili kutoka nchi ilikosajiliwa;

(v) Kuwasilisha Muhtasari wa kikao cha wanachama waanzilishi;

(vi) Kuwasilisha barua ya utambulisho (Recomendation Letter) kutoka kwa Msajili Msaidizi wa Halmashauri au Mkoa Ofisi ilipo.

NB: Usajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (Local & International - NGOs), hufanyika kwa njia ya mfumo wa kielekroniki kupitia tovuti: nis.jamii.go.tz

C. ADA ZA USAJILI

Mashirika ya Kimataifa - USD 350

Mashirika ya Ndani :-

  • Ngazi ya Kitaifa - Tsh. 115,000/=
  • Ngazi ya Mkoa - Tsh. 100,000/=
  • Ngazi ya Wilaya - Tsh. 80,000/=
  • Ushuru wa Stempu za TRA; Shirika la ndani (Stamp Duty) - Tsh. 1,500/=
  • Ushuru wa Stempu za TRA; Shirika la Kimataifa (Stamp Duty) - Tsh. 4,500/=

D. MAHITAJI BAADA YA USAJILI

(i) Kulipa Ada ya mwaka 50,000/= kwa Mashirika ya ndani na $100 kwa Mashirika ya Kimataifa. Malipo ni sambamba na uwasilishaji wa Ripoti za Mwaka za Utendaji kazi pamoja naTaarifa ya Fedha iliyokaguliwa. Malipo hufanyika kati ya Tarehe 01 Januari hadi 15 Aprili. Kushindwa kutimiza takwa hili la kisheria hupelekea kulipa faini ya Tsh. 100,000/= kwa Mashirika ya Ndani na $300 kwa Mashirika ya Kimataifa.

(ii) Shirika ambalo litashindwa kulipa ada na kushindwa kuwasilisha taarifa za mwaka za utendaji kazi kwa miaka miwili mfululizo litakuwa limepoteza sifa za usajili na litatakiwa kufutwa kwa mujibu wa sheria.