Matangazo
HATI YA KUKUSUDIA KWA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI
Hii ni kujulisha kuwa umekiuka sheria na masharti ya usajili kama hapa chini:-
(I) Kushindwa kuwasilisha ripoti ya mwaka kwa miaka miwili mfululizo kinyume na kifungu cha 29 (1) (a) na (b) cha sheria ya Mashirika Yasiyo Ya Kiserikali Na. 24 ya 2002;
(II) Kushindwa kulipa ada za mwaka za Shirika Kinyume na kifungu cha 38(2) (b) cha sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali na. 24 of 2002 kinachosomwa pamoja na Kanuni ya 10 ya Kanuni ya Kanuni za Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ya mwaka 2004 na Jedwali la Pili la Kanuni Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (Marekebisho) ya 2014.
UNAARIFIWA kwamba, kwa mujibu wa kifungu cha 24 9(1) na (2) cha Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24 ya 2002, unatakiwa kutoa sababu zinazojitosheleza kwa maandishi kwa ofisi ya Msajili kabla ya tarehe 30 Juni, 2022.
Orodha ya Masharika yanayokusudiwa kufutwa yanapatikana kwenye tovuti www.jamii.go.tz
Vickness G.Mayao
MSAJILI WA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI