Katibu Mkuu wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum Dkt. John Jingu akishiriki katika Mkutano wa kimataifa unaohusisha wajumbe wa nchi jumuiya za umoja wa kimataifa kwa lengo la kujadili nafasi ya mwanamke katika nchi zao ikiwa ni miaka 30 baada ya maazimio ya Beijing Machi 13, 2025 Jijini New york Marekani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiongea na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima (Mb) mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Sheikh Abeid Amri kwa mkoani Arusha ajili ya Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake Machi 8, 2025
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima (Mb), akisalimiana na wananwake wakati wa wa Kongamano laWananwake kanda ya Ziwa lililofanyika Machi 2, 2025, mkoani Geita.
Waziri wa Ulinzi na jeshi la kujenga Taifa Dkt. Stargomena Tax akiwa na viongozi wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wanawake na Makundu Maalum, Viongozi wa Mkoa wa Arusha pamoja na wageni Waalikwa kwenye Kongamano la Wananwake kanda ya Kaskazini lilifanyika Machi 6, 2025 Kwenye ukumbi wa AICC jijini Arusha.
Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) ambaye pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb) akihutubia kwenye Kongamano la Wanawake wa nyanda za Juu Kusini lililofanyika March 5, 2025 Mkoani Mbeya.
Mgani rasmi wa kongamano la Wanawake Kanda ya Kati Mhe. Anna Makinda, Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akifurahia ngoma ya kabila la Wagogo ikitumbuiza wakati wa kongamano hilo lililofanyika Machi 4, 2025 jijini Dodoma,
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb) (aliyesimama Katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa Kongamano la Wanawake kanda ya Mashariki lililofanyika Machi 4, 2025 katika ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Phillip Mpango akikabidhi jiko la gasi wakati wa hafla ya Kongamano la Wanawake wa kanda ya Magharibi Mkoani Kigoma.
Kwaya ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum ikitumbuiza katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake iliyofanyika Machi 08, 2025 jijini Arusha.